MKOA WA IRINGA WAZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI WA MITI- JUMLA YA MICHE MILIONI 41 KUPANDWA
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa ikiongozwa na Mwenyekiti Mheshimiwa Daud Yassin imezindua Kampeni ya Upandaji wa Miti katika Mkoa wa Iringa ambapo Uzinduzi umefanyika Wilaya ya Mufindi na lengo la Mkoa ni kupanda Miche ya Miti Milioni 41.
“ Miti ikiwepo mazingira yanaimarishwa, mvua zinanyesha , hali ya hewa inakuwa bora, tujitahidi sana kupanda miti tunataka Mkoa wa Iringa uendelee kuwa wa Kijani . Tuwapongeze Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na TFS kwa Miche hii ambayo ipo tayari imetolewa ili ianze kupandwa hasa kipindi hiki cha mvua.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa akiwa ameongozana na Kamati ya Siasa Mkoa wa Iringa katika Uzinduzi huo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego amesema kuwa miche ya miti ipo tayari kupitia TFS hivyo amezitaka Halmashauri zote kwa mkoa wa Iringa kuhakikisha wanapanda miti ili kufikia malengo kwani huu ni utamaduni wetu watanzania.
Akisoma taarifa ya Upandaji wa Miti kwa Mkoa wa Iringa Dkt. Bahati Golyama amesema kuwa kwa mwaka 2024 lengo la Mkoa ni kupanda miche Milioni 41.5. Amesema kwa mwaka 2022/2023 mkoa wa Iringa kupitia halmashauri zake ilipanda miche ya miti Milioni 38.9 ambapo Halmashauri ya Mji Mafinga ilifanikiwa kupanda miche milioni 1.7.
Dkt. Golyama amesema changamoto kubwa katika utunzaji wa miti na uhalibifu wa mali na uchumi ni moto ambapo kwa kipindi kilichopita jumla ya matukio 1800 ya moto yaliripotiwa. Hivyo ni vema kutokuwasha
Moto na kujua madhara yatokanayo na moto.
Kampenzi ya uzinduzi wa Upandaji
Wa Miti Mkoa wa Iringa imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Dkt. Linda Salekwa Kamati yq Ulinzi na Usalama
Wilaya ya Mufindi, Viongozi wa Taasisi mbalimbali Wilayani Mufindi Mkurugenzi Mji
mafinga na Wakuu wake wa Divisheni na Vitengo.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano
serikalini- Mafinga TC
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano- Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.