Ni wajibu wetu kuhakikisha Mapato yanakusanywa na hayavuji, tuhakikishe Timu za Ukusanyaji Mapato zinafanya kazi kwa kufuata uadilifu. Na uaminifu mkubwa huku tukizifuatilia kwani hakuna haki bila wajibu”
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi. Fidelica Myovella alipokuwa akizungumza na Kamati ya ukusanyaji mapato katika Halmashauri ya Mji Mafinga lengo likiwa ni kupanga mikakati ya kukusanya Mapato na kubuni vyanzo vipya vya mapato.
“ Kamati hii lazima itafanya kazi na Timu za ukusanyaji Mapato ngazi ya Kata na Mitaa, niwatake kuhakikisha mnazisimamia Timu hizi kwa ukaribu na kuhakikisha wanafuata maadili katika ukusanyaji mapato, tutahakikisha Timu za Ukusanyaji mapato zinajengewa uwezo ili ziweze kufanya kazi kwa weledi mkubwa na kuleta Tija”
Katika kikao hicho Mikakati mbalimbali bunifu imepangwa ili kuweza kuongeza mapato ya Halmashauri lengo likiwa ni kutoa huduma bora kwa jamii na kuongeza mapato ya Serikali.
Kikao cha kupanga Mikakati ya Ukusanyaji Mapato kimehudhuriwa na Mwenyekiti wa Kamati ambaye ni Mkurugenzi Mji Mafinga Bi Fidelica Myovella Katibu wa Kamati hiyo Afisa Mipango ndugu Peter Ngusa na wajumbe wengine ambao ni:-Mkurugenzi -Mwenyekiti
Afisa Mipango -Katibu,Mhasibu wa Mapato
Mweka Hazina ,Afisa TEHAMA , Afisa Biashara
Mwanasheria, Afisa Mipango miji,
Afisa maendeleo ya Jamii , Afisa Habari na Afisa Mazingira
Na Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.