“Lengo la Serikali ni kuhakikisha tunalea kizazi bora ambacho kitasaidia kuinua uchumi wa taifa kwa kuhakikisha changamoto inayotokana na Lishe inaisha katika Jamii”
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mji Mafinga Bi. Fidelica Myovella alipokuwa akifungua kikao cha Lishe kwa robo ya pili 2024/2025 kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Mafinga.
Afisa Lishe Halmashauri ya Mji Mafinga Bi. Josephine Kazungu amezitaja kazi zilizofanywa kuwa ni:-
Ukaguzi wa viwanda vinavyorutubisha sembe
Huduma kwa mama mjamzito
Matibabu ya utapiamlo mkali
Maadhimisho ya siku za afya na Lishe
Usimamizi shirikishi wa shughuli za lishe katika vitu o vya kutolea huduma
Ufuatiliaji wa watoto wenye utapiamlo kwenye Jamii
Utekelezaji wa afua za lishe
Usimamizi shirikishi wa shughulu za lishe mashuleni
Kikao hicho cha kujadili taarifa za lishe na kuweka mikakati kimehudhuriwa na wadau mbalimbali ambao ni wataalamu wa Lishe, viongozi wa dini na wataalamu wa Mji Mafinga.
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.