“Watumishi hakikisheni mnaizungumzia vizuri Serikali hasa katika Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa kwenye Kata zenu, msikae kimya semeni ili wananchi wajue kwa kushirikiana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini tumieni kitengo cha Mawasiliano ili kitangaze Miradi iliyokwenye kata zenu” Ayoub Kambi, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Mafinga.
Akizungumza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu, Ayoub Kambi kwenye ziara yake kusikiliza changamoto za watumishi kwa Kata za Rungemba na Saohili amesema Miradi mingi inayotekelezwa kwenye Kata ni mingi kama Ujenzi wa Madarasa, Shule,nyumba za walimu na vituo vya Afya toeni taarifa nini kinafanyika ili kitengo cha Mawasiliano kichukue taarifa na zitangazwe.
“ Nimepokea changamoto zenu na nitazifanyia kazi na ndo mana nimekuja na wataalamu wangu ili lile linaloweza kutatulika liishe na Yale yanayohitaji ufuatiliaji nayachukua kwa Utekelezaji mkifanya kazi kwa uwazi hakutakuwa na malalamiko Kwa Serikali . Pia nimeshatoa maekezo kuwa Mwananchi akifika ofisini kwenu apewe huduma haraka aondoke.Asikae muda mrefu kusubiri huduma, sio sawa”
Amesema wananchi wengi hawachangii Miradi ya Maendeleo kwa sababu watendaji hawasomi mapato na matumizi hivyo kufanya wananchi kukosa Imani watendaji. Hivyo ameagiza mapato na matumizi yasomwe na mapokezi ya fedha yabandikwe kwenye mbao za matangazo.
Kikao kimehudhuriwa na Watumishi wote Kata ya Rungemba na Saohill, Wataalamu kutoka Makao Makuu Idara ya Utawala, Elimu Msingi, Sekondari , Afya na Mipango.
Ziara ya Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu Ayoub Kambi Ni ziara ya kimkakati ambayo imeanza tarehe 21/6/2023 mpaka tarehe 6/7/2023.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-MAFINGA TC
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.