Mkurugenzi MJI Mafinga Bi Fidelica Myovella akiwa ameambatana na Afisa Mipango Ndugu Peter Ngusa na Mhandisi wa Halmashauri ya MJI Mafinga Christopher Nyamvugwa wamefanya Ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo lengo likiwa ni kuhakikisha hakuna changamoto yoyote inayosababisha Miradi isitekelezwe kwa wakati na kuhakikisha Miradi inajengwa kwa Ubora na kukamilika kwa wakati.
Miradi iliyopitiwa ni Mradi wa Ujenzi wa Madarasa 2 katika Shule ya Sekondari Itimbo Madarasa yanayojengwa kwa Mapato ya Ndani ambapo kiasi kilichotolewa na Halmashauri ni Milioni 50.
Aidha Mkurugenzi na Timu yake wametembelea Ukamilishaji wa Mabweni mawili katika Shule ya Sekondari Ndolezi ambayo yamekamilika kwa asilimia 90 , amewaomba kuhakikisha yanakamilika kwa wakati ili yaweze kutumika kama ambavyo yamelengwa .
Aidha katika Kata ya Isalavanu Mkurugenzi amejionea ukamilishaji wa darasa katika Shule ya Msingi Mamba na kushauri kukamilisha madawati ili yawe rafiki kwa matumizi ya wanafunzi.
Pia katika Kata hiyo yanajengwa madarasa 2 ambapo Halmashauri imepeleka kiasi cha shilingi milioni 50 kutoka katika Mapato ya ndani ili kujenga madarasa hayo katika Shule tarajiwa ya Sekondari ambayo itakuwa Mkombozi kwa wanafunzi wa eneo hilo na Kata za Jirani.
Aidha amewataka Wataalamu kusimamia mafundi ili UJENZI uwe kwenye ubora na thamani ya Majengo na fedha zilizowekwa zifanane na majengo yakamilike kwa wakati.
“ Mafundi wanafanya kazi nzuri lakini tusiwaache peke yao lazima tuwasimamie kwa ukaribu ili ikitokea changamoto tuibaini haraka tusisubiri viongozi waje wabaini changamoto zetu”
Mradi mwingine uliotembelewa ni UJENZI wa madarasa 2 katika Kata ya Bumilayinga ambapo amewataka wasimamizi ngazi ya Kata kusimamia vizuri ukamilishaji wa Madarasa hayo ili kuweza kupata usajili mapema mwakani.
Sima BINGILEKI
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.