Baada ya kuvuna maparachichi bora kwenye shamba hili tunaendelea kutoa matunda yote madogo yaliyosalia kwenye miche, kulimia miche, kuweka mbolea ili mazao yanayoanza yaanze na kukua pamoja yakiwa na ukubwa unaolingana na yenye ubora kwaajili ya kupata mazao bora huku tukiruhusu umwagiliaji wa matone kuendelea”
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi, Fidelica Myovella alipokuwa akifanya utuatiliaji katika shamba la parachichi linalomilikiwa na Halmashauri lenye hekari 50 lililo katika Kata ya Changarawe
Amesema moja ya kipaumbele kwa Idara ya kilimo ni Shamba la parachichi ambapo kimechimbwa kisima chenye thamani ya shilingi 22,000,000/- kutoka matapo ya ndani ili kuboresha shamba la parachichi ikiwa ni kuongeza mapato ya Halmashauri na Shamba darasa kwa wananchi wanaopenda kujifunza kilimo cha parachichi.
Akizungumza Mkuu wa Idara ya Kilimo mifugo ndugu Evance Gabriel Msosa akiwa ameambatana na wataalamu wa Idara hiyo amesema shamba limevunwa matunda yote lengo likiwa ni kuruhusu matunda mapya kukua pamoja na ukubwa sawa ili kuongeza ubora wa mazao.
Amesema shamba lina mfereji wa maji, kisima na matenki kwaajili ya kuhifadhia maji hasa kipindi cha kiangazi hivyo amesema maandalizi haya yanalenga kupata mazao bora
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi Fedelica Myovella akifatilia zoezi la uvunaji wa parachichi katika shamba la Halmashauri.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.