Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga, Bi. Fidelica Myovella, amefanya ziara ya kuwatembelea wanamichezo kutoka Halmashauri ya Mji Mafinga wanaoshiriki michezo ya Shirikisho la Michezo ya Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA) inayoendelea kufanyika jijini Tanga.
Pia amewapongeza kwa hatua waliyofikia mpaka sasa kwa michezo ambayo tayari imefanyika kwa wanawake volleyball kuongoza katika kundi waliopo na Mchezaji Tonely Mkimbo kuibuka mshindi wa kwanza Riadha Mita 1500 hatua ya makundi kwa kutoa motisha ya kiasi cha fedha na amehaidi kuendelea kutoa fedha kwa kila seti ya Mchezo watakaoshinda atatoa 100,000/= pia amewatoa hofu kuwa uongozi wa halmashauri upo nyuma yao na uko tayari kuendelea kuwasaidia katika kila hatua.
Mashindano ya SHIMISEMITA yanatarajiwa kumalizika tarehe 29/08/2025 na timu ya Mafinga inaendelea na maandalizi ya mechi zijazo kwa ari kubwa.
Na,
Anna Mdehwa,
Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.