MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA BI, FIDELICA MYOVELA AKABIDHI BENDERA YA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA KWA TIMU YA HALMASHAURI INAYOKWENDA KUSHIRIKI MICHEZO YA SHIMISEMITA
Posted on: August 15th, 2025
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi, Fidelica Myovela akabidhi Bendera ya Halmashauri ya Mji Mafinga kwa timu ya Halmashauri inayokwenda kushiriki michezo ya SHIMISEMITA inayotarajiwa kuanza Tarehe 15/08/2025 mpaka 29/08/2025 Mkoani Tanga.
Akizungumza na wanamichezo wanaowakirisha Halmashauri ya Mji Mafinga kuelekea Tanga amewapongeza Kwanza kwa kujitokeza kushiriki na pia amewaasa wakaoneshe vipaji na kuwa na nidhamu kwa kipindi chote hicho cha michezo na kuwatakia kheri kwenye mashindano hayo.
Kwa upande wake Afisa Utumishi Mkuu Charles Mwaitege amesisitiza ushirikiano na nidhamu kwa wanamichezo kwa kipindi chote ambacho watashiriki michezo Mkoani Tanga.
Kauli Mbiu ya Shirikisho la Michezo ya Serikali za Mitaa Tanzania (SHIMISEMITA) Jitokeze Kupiga Kura Kwa Maendeleo Ya Michezo.