uhakikishe tunawapa ushirikiano mafundi na tuwe nao karibu ili waweze kumaliza kazi kwa wakati na kwa ubora mkubwa ili kusiwepo kasoro katika ukamilishaji wa Miradi tunayoitekeleza kwa mfano, Maabara hii katika Shule ya Sekondari Nyamalala hadi kukamilika kwake itagharimu kiasi cha shilingi Milioni 61 inajengwa na fedha za mapato ya ndani ambazo ni kodi za wananchi hivyo lazima tuzisimamie zilete manufaa kwa jamii yetu”
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mji Mafinga Bi Fidelica Myovella alipokuwa akifanya ziara ya ufuatiliaji kuona maendeleo ya Miradi na chamgamoto zinazo wakabili mafundi kwenye utekelezaji wa Miradi hiyo.
Jumla ya Miradi 7 ilipitiwa na Mkurugenzi wa Mji Mafinga ukiwamo mradi wa:-
Ukamilishaji Shule ya Sekondari Upendo
- Ujenzi wa jengo kituo cha afya Ifingo
- Ukamilishaji shule ya Amali bwalo, jiko na mabweni
- Ukamilishaji wa Maabara Shule ya Sekondari Nyamalala
- Ujenzi wa Bwalo Chief Mkwawa English medium
- Ujenzi nyumba 2 in 1 Shule ya Sekondari Ndolezi.
Akizungumza Mkurugenzi Mji Mafinga Amesema Fedha zinazoletwa kutoka Serikali Kuu ni nyingi ambapo ndoto ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona wanafunzi wa Kitanzania wanapata elimu bora katika mazingira wezeshi na Sekta nyingine zinaimarika katika miundombinu ya majengo, vifaa na watoa huduma ili wananchi wapate huduma bora naya haraka.
Nyumba ya Walimu 2 in 1 katika Shule ya Sekondari Ndolezi inajengwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu( SEQUIP) ambapo gharama za Mradi ni shilingi milioni 100.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Mafinga TC
Sima Mark Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi waa shule ya Amali.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.