Mkurugenzi MJI Mafinga Bi. Fidelica Myovella amehudhuria Mkutano wa Wananchi Katika Kijiji cha Itimbo Kata ya Rungemba Mkutano ulioitishwa na Diwani wa Kata ya Rungemba ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Mji Mafinga Mheshimiwa Samwel Mwalongo lengo likiwa ni kusikiliza Kero za Wananchi na kutoa taarifa za Utekelezaji Miradi ya Maendeleo katika Kata ya Rungemba.
Akizungumza kuhusu fedha za Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Kata Hiyo Bi. Fidelica Myovella amesema Kupitia Mapato ya Ndani Halmashauri imeleta Milioni 50 kwaajili ya Ujenzi wa Madarasa 3 Shule ya Sekondari Itimbo na Umaliziaji wa Darasa moja, zaidi Halmashauri imetenga imeleta kiasi cha Shilingi milioni 30 kwaajili ya Ukamilishaji wa Jengo la Wazazi katika Zahanati ya Kitelewasi kutoka Mapato ya Ndani
Aidha amewashukuru wananchi wa Kata ya Rungemba kwa Ushiriki Mzuri wa Mapokezi ya MWENGE wa UHURU 2025 katika Shule ya Msingi Rungemba na ushiriki wa Miradi ya Maendeleo.
Sima Mark Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.