Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego amekabidhi pikipiki 216 kwa Maafisa Ugani wa Mkoa wa Iringa ambazo zimetolewa na wizara ya kilimo, lengo likiwa ni kuleta mapinduzi ya kijani katika sekta ya kilimo cha chakula na kilimo cha kibiashara.
Amesema Serikali ya Awamu ya sita imedhamiria kuinua na kuleta mapinduzi katika Sekta ya kilimo. Hivyo lengo la Mheshimiwa Rais ni kuona wakulima wanapewa ushauri wa Kitaalamu kwa ukaribu ili kuinua hali zao za kiuchumi kupitia sekta ya kilimo.
“ Maafisa Ugani tuhakikishe pikipiki hizi zinaleta Mapinduzi ya kijani, kila mmoja atimize wajibu wake, anachotaka kuona Mheshimiwa Rais ni kuwasaidia wakulima kuwashauri kitaalamu”
Nae Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na uzalishaji Mkoa wa Iringa, Ndugu Elias Luvanda amesema Mkoa wa Iringa una jumla ya Maafisa Ugani 230 na mahitaji ni maafisa Ugani 444 hivyo upungufu ni Maafisa Ugani 214, hivyo pikipiki hizi zilizotolewa na Wizara ya Kilimo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua sekta ya kilimo kwa wataalamu sasa watawafikia wakulima popote walipo hususan kwenye Mkoa wa Iringa.
Amesema Wizara ya Kilimo italeta Sare kwaajili ya Maafisa Ugani hao,vifaa vya kupimia (Soil Scaner )ubora wa udongo kwaajili ya kilimo na kutakuwa na daftari maalumu la kilimo katika kila kijiji ambalo litawatambua wakulima wote kati eneo husika, kilimo kinachofanyika, na ushauri unaotolewa ili kila mmoja atimize wajibu wake.
Katika pikipiki zilizotolewa 216, Halmashauri ya Mji Mafinga imepokea jumla ya pikipiki 16 kwaajili ya maafisa ugani 16 walio katika Halmashauri hiyo.
Akizungumza Mkuu wa Idara ya Kilimo Ndugu, Francis Maghembe amesema kuwa pikipiki zilizopokelewa zitasaidia kuwafikia wakulima hadi ngazi ya kijiji hivyo wamemuahidi Mheshimiwa Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wakulima katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga wanafikiwa na kushauriwa ili kukuza na kuongeza mapinduzi ya kijani katika Mkoa wa Iringa.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGA TC
Sima Bingileki
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga TC
@samia_suluhu hassan
@halimadendego
@ortamisemi
@daud_yasin_mlowe
@angellah_kairuki
@wizara_ya kilimo
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.