MKUU WA MKOA WA IRINGA MHESHIMIWA HALIMA DENDEGO ATETA NA WAWEKEZAJI WA MAZAO YATOKANAYO NA MISITU – MAFINGA.
“Hatuwezi kuona zao la Mbao linachezewa, tutahakikisha tunalipambania zao hili kwani bila miti Hakuna Iringa”
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego alipokuwa akisikiliza changamoto wanazokabiliana nazo wawekezji na wafanyabiashara wa mazao ya misitu Wilaya ya Mufindi katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Mafinga.
Amesema lazima tutafute shida iko wapi, kwanini zao la mbao lishuke bei wakati mahitaji ya mbao ni makubwa , lazima tutafute tatizo, Kuna watu lazima hawalipi mapato wanatumia njia za panya kuchukua mbao kwa wananchi lakini mwisho lazima mbao hizo zije sokoni hivyo hata kwa bei ya hasara watauza ili mzigo uishe na kwa wale wanaolipa mapato watakutana sokoni hivyo kufanya bei ya zao hilo kushuka.
Naye Mwenyekiti wa UWASA Chama Cha Wavunaji SAOHILL Ndugu, Cristian Ahiya amesema kuwa tatizo kubwa la kushuka kwa zao la mbao ni kutokana na baadhi ya wananchi wanaouza misitu yao kwa bei ya hasara ikiwa haijakomaa ili kutatua matatizo yao hivyo kufanya kushuka kwa bei.
Matelekeza Chang’a Mjumbe wa UWASA amesema kuwa shida ni wavunaji wa kawaida kuvuna miti ambayo haijakomaa hivyo kushusha bei ya soko na kuuza kwa hasara.
Mkuu wa Mkoa amesema changamoto hii anaifanyia kazi na majibu yatawafikia walengwa, lengo wafanyabiashara wafanye biashara kwa haki na Serikali ipate mapato yake.
Wilaya ya Mufindi inajumla ya viwanda visivyopungua 23 vya uzalishaji wa zao la mbao na viwanda hivyo bado havitoshelezi mahitaji ya soko.
Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa Bi Halima Dendego ametambulisha ujio wa Karibu Kusini ambao unalengo la Kutangaza vivutio vya utalii Nyanda za Juu na Utamaduni na kuunga mkono Royal Tour
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Mafinga TC
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.