Hakikisheni Miradi hii inakamilika katika Muda uliopangwa na thamani ya Mradi iendane na fedha iliyotumika, Mpaka hapa mlipofikia kwenye hatua ya ukamilisha thamani ya
Miradi inaonekana na ninaimani mtaikamilisha kwa wakati kama ambavyo maelekezo yanasema.Jukumu letu ni kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake kubwa anazofanya kuhakikisha fedha zinakuja kwa wakati “
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego alipofanya ziara katika Halmashauri ya Mji Mafinga kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Miradi iliyotembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Dkt Linda Salekwa na kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya mufindi ni Mradi wa Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Ndolezi( SEQUIP) ambayo inajengwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu kiasi cha Shilingi 583,180,028 na unatarajiwa kukamilika tarehe 30/10/2023
Majengo yaliyopo katika Shule hii ni pamoja na:-
Vyumba 8 vya madarasa
Maabara tatu
Jengo la TEHAMA
Kichomea Taka
Jengo la Matundu 10 ya vyoo wasichana
Jengo la Matundu 8 ya wanafunzi wa wavulana
Maktaba 1
Chumba cha Computer 1
Aidha Mkuu wa Mkoa pia ametembelea ujenzi wa Jengo la kuhifadhia Maiti( Mortuary) katika Hospitali ya Mji Mafinga ambapo chanzo cha Fedha za ujenzi ni mapato ya ndani ya Hospitali ya Mji Mafinga ambapo mpaka sasa fedha zilizotengwa ni shilingi milioni 66.750
Akizungumza Mganga Mkuu
Wa Halmashauri ya Mji Mafinga Dkt. Chitolela Bonaventulla amesema kuwa jengo la kuhifadhia Maiti lilipangiwa fedha kwa Awamu mbili kutoka mapato ya ndani ya Hospitali ya Mji Mafinga. Ambapo awamu ya kwanza zilitolewa Milioni 41.750 na awamu hii jengo lipo hatua ya umaliziaji ambapo zimetengwa shilingi Milioni 25.
Amesema lengo la kujenga jengo jipya la kuhifadhia Maiti( Mortuary) katika Hospitali ya Mji Mafinga ni baada ya kuona uchakavu wa jengo la zamani,kutoa huduma kwa wananchi kuleta miili ya ndugu zao wakitokea Maeneo jirani Mji wa Mafinga kwani jengo linauwezo wa kuchukua makabati manne na kulitoa usoni mwa hospitali kuliweka nyuma ya hospitali kwa vigezo vya WHO zaidi ni kupunguza muingiliano uliokuwepo nyuma.
Jengo linatarajiwa kukamilika mwezi Novemba 2023.
Ziara pia imhudhuriwa na waheshimiwa Madiwani, Mkurugenzi Mji Mafinga Ndg. Ayoub Kambi pamoja na wataalamu wa Halmashauri ya Mji Mafinga.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Setikalini- Mafinga Tc
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.