"Baada ya zoezi hili nina Imani hakutakuwa na mgomo tena kutoka kwa wafanyabiashara Mji Mafinga katika Soko la Mafinga, nimemsikiliza Mfanyabiashara mmoja mmoja katika vibanda 405 kusikiliza matakwa yao kuhusu ulipaji wa kodi na tumekubaliana”
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Peter Serukamba @serukamba amefanya maamuzi hayo kulingana na uhalisia wa kibanda na Biashara inayofanyika.
“ Baada ya kupita na kuzungumza na Wafanyabiashara kuna niliowapunguzia kodi na kuna ambao watatakiwa kulipa Kama ilivyo kuwa awali. Serikali inaleta Fedha nyingi hivyo ni lazima tukusanye mapato ili kuwahudumia wananchi sitataka kusikia tena kuna mgomo. Hakikisheni mnalipa kodi ili kuongeza mapato.
Katika zoezi hilo wafanyabiashara ambao hawajalipa kodi kabisa wamezungushiwa utepe vibanda vyao ili wakalipe siku ya jumatatu na wakishindwa basi vibanda vyao vitagawiwa kwa wafanyabiashara wengine,
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.