Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mheshimiwa Peresi Magiri kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego amemkabidhi Mwenge wa Uhuru 2023 Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa leo tarehe 1/5/2023.
Akitoa taarifa ya Mkoa Mheshimiwa Peresi Magiri amesema katika Mkoa wa Iringa Mwenge utakimbizwa kwenye Wilaya 3, Halmashauri 5 kwa umbali wa kilomita 719 ambapo jumla ya Miradi ya Maendeleo 31 yenye thamani ya shilingi 63,194,840,527.88 itapitiwa na mwenge wa uhuru kwaajili ya ufunguzi, uzinduzi, kuweka jiwe la msingi na kukagua.
Mwenge wa Uhuru umepokelewa Mkoa wa Iringa tarehe 1/5/2023 na tarehe 6/5/2023 utakabidhiwa Mkoa wa Morogoro.
Halmashauri ya Mji Mafinga Itakimbiza Mwenge tarehe 5/5/2023.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGA TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.