ALIYOSEMA MKUU WA WILAYA YA MUFINDI MHE. DKT. LINDA SALEKWA WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAZEE WA WILAYA YA MUFINDI- MAFINGA
-Nawashukuru Viongozi wa dini na viongozi wa kimila kufanya dua na kuhakikisha Mufindi ni salama.
-Moja ya Mkakati wa Wilaya ya Mufindi ni kuhakikisha maadili yanafuatwa.
- Ofisi ya Mkuu wa Wilaya itahakikisha fedha zote zinazotolewa na Serikali zinatekeleza majukumu yaliyo pangwa.
- Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mufindi itahakikisha inasimamia haki za wazee.
- Taifa linatambua mchango mkubwa wa wazee katika kusimamia nchi.
-Wazee ni hazina, tuhakikishe tunatimiza wajibu wetu na kusimamia nafasi zetu katika kutunza maadili ya vijana wetu.
-Katika kupambana na mmomonyoko wa maadili tunategemea sana wazee.
-Wazee mnawajibu wa kuwaasa vijana katika kusimamia maadili.
- Vitendo vya Ukatili ushoga havikubaliki kwenye jamii yetu. Tuvipinge.
-Tutahakikisha wote wasio fata maadili wanashughulikiwa katika kutoa huduma kwa wazee, hasa kwenye sekta za Afya. Tuwahudumie na kuwathamini wazee wakija kutaka huduma kwetu.
- Wakurugenzi hakikisheni kwenye vituo vya Afya wazee wanapewa umuhimu na kipaumbele katika kuhudumiwa
- Wazee wasipange foleni sehemu yoyote wahudumiwe haraka.
- Wazee mkiona hampewi haki na kuhudumiwa kwa haki toa taarifa haraka taja eneo na wapi tutashughulika na huyo muhusika.
- Wahusika wa barabara wahakikishe matuta yanawekwa sehemu zenye mikusanyiko ya watu.
- Wawekezaji wageni wapewe misimamo ya wilaya na maadili ya watanzania ili waendane na jamii wanazoishi nazo na mikataba ya wafanyakazi kwenye viwanda ifuatiliwe ili kulinda haki za wafanyakazi.
- Suala la utapiamlo ni mkakati wa Wilaya na Mkoa tunahakikisha tunatokomeza tatizo hili.
- Tumeweka msisitizo kila shule mtoto mwanafunzi ale chakula cha mchana na wazazi wachangie chakula ili watoto wapate chakula wanapokuwa shuleni.
- Tumeagiza kila shule iwe na bustani ya mboga mboga hii ni katika jitihada za kuzuia utapiamlo na kuboresha lishe.
- Tunaomba wazee mtusaidie kuwahimiza wazazi kuchangia chakula mashuleni ili kupambana na tatizo la lishe.
- IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGA
- Sima Bingileki-Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.