• Malalamiko |
    • Wasiliana na sisi |
    • Maswali |
    • Baruapepe |
Mafinga Town Council
Mafinga Town Council

Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mafinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Organization Structure
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Kilimo na umwagiliaji
      • Fedha
      • Mipango na Takwimu
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Afya
      • Ardhi na Maliasili
      • Community Development,Social welfare Gender and Youth
      • Water
      • Work
    • Vitengo
      • Community
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Huduma za Kisheria
      • Biashara
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa madiwani
    • Kamati Za Kudumu Za Halmashauri
      • Fedha Na uongozi
      • Mipangomiji Namazingira
      • Uchumi, Fedha Na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana Na Mwenyekiti
  • Miradi Mbalimbali
    • Progressive projects
    • Itakayo Tekelezwa
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Machapisho ya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Makitaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Malalamiko

Mkuu wa wilaya ya mufindi aokoa ekari 643 za wananchi zilizoporwa na mwekezaji

Posted on: September 20th, 2018


Mkuu wa wilaya mufindi mh. Jamhuri william amemaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda wa miaka kumi na mbili baina ya mwekezaji Tom Duvile mkurugenzi wa Highland Holding Company dhidi ya wananchi wa kinyanambo na kijiji cha kikombo ambapo zaidi ya ekari 643 zilizonunuliwa kinyume na utaratibu na sheria zimerudishwa kwa wananchi na halmashauri ya mji mafinga.

Ekari zilizorejeshwa ni 396 kwa wananchi kumi na saba walalamikaji kutoka katika kata ya kinyanambo, ekari themanini na saba za kijiji cha kinyanambo, ekari 79.9 za kijiji cha kikombo zimerudishwa kwa halmashauri ya mji mafinga na ekari 80.1 zimerudishwa kwa wananchi mbalimbali wa kijiji cha kikombo.

Mh. William alibainisha kuwa mara baada ya kukabidhiwa ofisi ya ukuu wa wilaya alikutana na malalamiko ya wazee kumi na saba kutoka mtaa wa kinyanambo ambapo viongozi waliopita walijaribu kuutatua lakini haukufikia muafaka ndipo yeye akaamua kuunda tume ya wataalamu mbalimbali wakiwemo wa ardhi kupitia upya madai ya hao wazee na pia kufika katika eneo la ardhi linalolalamikiwa na mwekezaji huyo.

Mgogoro wa ardhi kati ya wananchi kumi na saba wa kata ya kinyanambo dhidi ya mwekezaji ndugu Tom Duvile ambaye alivamia mashamba ya wananchi waliyopewa na serikali ya kijiji cha kinyanambo mwaka 1977 na lalamiko lao walipeleka kwa mkuu wa wilaya na mkurugenzi tangu mwaka 2006 hawakupatiwa ufumbuzi.

“Nimechukua muda mrefu sana kushughulikia tatizo hili nilikuwa nataka nione mimi mkuu wa wilaya nimekuja sasa ni miaka mitatu imepita lakini wenzangu walitangulia niliona walitatua vipi mgogoro huu na walikwama wapi kwa hiyo nilikuwa nataka kujiridhisha na ndio maana suala hili limechukua muda mrefu sana” alisema mh. william

Mgogoro huu ulishatolewa maamuzi na viongozi mbalimbali akiwepo aliyekuwa mkuu wa wilaya mufindi bi. Evarista kalalu lakini maamuzi hayo hayakutekelezwa hivyo mgogoro huo uliendelea.

“Na leo hii nimekuja kutoa uamuzi kero yenu inaisha leo kwani waswahili husema mvumilivu hula mbivu, wananchi waliolalamika na mwekezaji kila mtu atapata anachostahili na hivyo ndio serikali yetu inavyofanya kazi kusikiliza kero na kuzitatua” alisistiza mh. william.

Aidha mkuu wa wilaya ameongeza kwamba katika mgogoro huo ofisi yake ilibaini kwamba taratibu za ununuaji wa ardhi hiyo zilikiukwa.

Ardhi inayolalamikiwa ni ekari 396 na hakuna mkutano mkuu ulioridhia uuzwaji wa ardhi hiyo.

Viongozi wa vijiji vya kinyanambo, kikombo na ndolezi walipaswa kuwasilisha mapendekezo ya mkutano mkuu wa kijiji unaoonesha kukubali mauzo ya ardhi hiyo kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya mufindi ambae angewasilisha kwenye kamati ya ugawaji ardhi ya halmashauri ya mufindi kwa vile ardhi iliyouzwa ilikuwa zaidi ya ekari hamsini zinazoruhusiwa kisheria kugawiwa na kijiji.

Kwa mujibu wa tume ya wataalamu iliyoundwa na mkuu wa wilaya ilibaini mapungufu ya msingi ikiwemo kijiji cha kikombo eneo ambalo uongozi wa kijiji walionesha ekari 79.9 ambalo limezidi kutolewa kwa mujibu wa sheria ambapo walitakiwa kutoa ekari zisizozidi hamsini.

Katika kijiji cha kinyanambo kijiji kilimpa mwekezaji ekari mia moja na ekari kumi na tatu ziliingia kwa ndugu mawazo chengula hivyo eneo la kijiji lililouzwa ni ekari themanini na saba ambalo pia lilitolewa kinyume na sheria ya ardhi ya vijiji.

Vilevile ndugu Tom Duvile alinunua jumla ya ekari 249.5 kutoka eneo la kijiji na wananchi mbalimbali lakini baada ya upimaji imebainika kuwa eneo la kinyanambo lina ukubwa wa ekari 483 na kufanya zidio la ekari 233.5

Kutokana na mapungufu hayo ofisi ya mkurugenzi wa mji mafinga ilimtaarifu kamishina wa ardhi kwa barua yenye kumbukumbu Namba HM/MF/A.30/76 ya 28/11/2016 na ushauri wake ulikuwa, mnunuzi afuate taratibu za umilikishaji wa ardhi ambazo zipo kisheria.

Mkuu wa wilaya mufindi baada ya kupitia hatua zote na kujiridhisha kwamba mwekezaji hakufuata taratibu na sheria za nchi ametoa maagizo ya utekelezaji ikiwemo maeneo yote yaliyouzwa bila kufuata utaratibu yarejeshwe mara moja kwa mamlaka husika au mwekezaji afuate upya taratibu za kupata maeneo hayo ikiwemo kujulikana na kituo cha uwekezaji tanzania (TIC).

“Naagiza eneo lipatalo ekari mia moja sitini na sita kuanzia sasa linarejeshwa kwa halmashauri ya mji mafinga, maeneo ambayo yalinunuliwa kwa wananchi bila kufuata sheria na taratibu katika kijiji cha kikombo hekari 80.1 kunzia sasa yanarudi kwa wananchi na Jumla ya ekari 396 kuanzia sasa hivi zinarudishwa kwa wananchi kumi na saba wa kata ya kinyanambo waliokuwa wakilalamika kwa muda mrefu” alisema mh. william

Aidha eneo ambalo mwekezaji Bwana Tom Duvile alinunua kwa familia ya Mdeka ekari 451 atabaki nazo na hilo ndio eneo alilopata kihalali lakini inaambatana na maelekezo yafuatayo kwa kuwa yeye ni raia wa kigeni basi afuate taratibu na sheria za kujimilikisha eneo hilo alisisitiza mh. william.

Mwekezaji bwana Tom Duvile kwa upande wake hakuridhika na maamuzi hayo huku akidai kuchangia ujenzi wa shule ya msingi katika kijiji cha kikombo kama ngao yake ya kuendelea kumiliki ardhi.

Kwa upande wake diwani wa kata ya kinyanambo mh. Chesco Lyuvale alimshukuru mkuu wa wilaya kwa kufikia maamuzi hayo kwani hata yeye toka ameingia udiwani amekutana na tatizo hilo na lilikuwa likimsumbua kwa muda mrefu hadi kulipeka kwenye chama chake ccm lakini lilikuwa bado haijatatuliwa.

“Ndugu zangu kwenye ukweli tuseme ukweli na kwenye haki ya mtu tusimame kwenye haki ya mtu, sisi hatujapanga kumuonea bwana Tom Duvile mimi nasema wewe mkuu wa wilaya umemaliza kama yeye haridhiki na maamuzi haya, sisi hatumlazimishi aridhike yeye anaweza kwenda mahakamani ili tukapambane huko kwenye vyombo vya sheria” alisema mh. Lyuvale.

Naye mwenyekiti wa mtaa wa gangilonga kata ya kinyanambo bwana Reginald Kivinge kwa niaba ya wananchi amempongeza mkuu wa wilaya kwa kufanya maamuzi hayo kwa faida ya wananchi wa kinyanambo, mafinga na tanzania kwa ujumla.

“Naomba nitoe pongezi kwa mh. mkuu wa wilaya, ni kweli jambo hili lilianza muda mrefu na ilifikia wakati wananchi tukawa kama tumeshindwa kuwa na majibu., kiukweli nichukue nafasi hii kukupongeza wewe, kwa kweli umewatendea haki wananchi wa kata ya Kinyanambo na umeweka historia katika uongozi wako hata siku unaondoka mafinga tutakukumbuka kwa tukio hili” alisema bwana kivinge.



Matangazo

  • NAFASI ZA MASOMO KWA SHULE YA CHIEF MKWAWA ENGLISH MEDIUM- HALMASHAURI YA MJI MAFINGA. NAFASI BADO ZIPO TUPIGIE January 29, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA YANAPATIKANA www.mafingatc.go.tz July 13, 2024
  • MJI MAFINGA YAVUKA LENGO UKUSANYAJI MAPATO YAKUSANYA ASILIMIA 113 KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024 August 14, 2024
  • MATOKEO YA DARASAM LA SABA 2024 YANAPATIKANA KWENYE TOVUTI YETU .www.mafingatc.go.tz October 30, 2024
  • View All

Habari mpya

  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI IMEENDESHA MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA KWA AWAMU YA PILI JIMBO LA MAFINGA MJINI

    May 02, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 KATIKA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA UMEPITIA JUMLA YA MIRADI 11 YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 3.1

    May 01, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 KATIKA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA UMEPITIA JUMLA YA MIRADI 11 YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 3.1

    May 01, 2025
  • MBUNGE WA MAFINGA MJI AKABIDHI MITUNGI YA GESI

    May 01, 2025
  • View All

Video

SENSA NI MAENDELEO
Video zaidi

Viungo Vya Haraka

  • Maelezo na Form Ya kiapo cha uadilifu
  • https://matokeo.necta.go.tz
  • Muongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya wananchi

Watembeleaji kidunia

world map hits counter

Idadi ya watu wanao tembelea Tovuti

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana na sisi

    Mafinga Town.

    Postal Address: Po.Box 76 Mafinga

    Simu: +255 262 772 393

    Mobile: 026-2772393

    Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.