Hakikisheni Utoaji wa chakula mashuleni kwa wanafunzi wote, bustani za mbogamboga na matunda mashuleni, Siku ya Lishe zinakuwa Ajenda za kudumu zinazojadiliwa kwenye vikao vya Maendeleo vya Kata zote katika Halmashauri ya MJI Mafinga lengo likiwa ni kupitia utekelezaji wa Mikataba ya Lishe na kupambana na udumavu na utapiamlo “
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa kwenye kikao cha kupitia Tathmini ya viashiria vya Mkataba wa Lishe kwa robo ya pili 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Mafinga na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa MJI Mafinga Bi.Fidelica Myovella, Wakuu wa Idara Maafisa Tarafa pamoja na Watendaji wa Kata zote 9 za Halmashauri.
Akiwasilisha taarifa Afisa Lishe Halmashauri ya MJI Bwana, Salum Atlas amesema Halmashauri ya Mji Mafinga chini ya Idara ya Afya imeendelea kuweka nia ya kutokomeza udumavu na utapiamlo kwa kuhakikisha inaweka bajeti kwa mwaka wa Fedha 2025/2026 ambapo jumla ya Tsh. 57,607,500 zitatumika kutekeleza afua za lishe ambapo jumla ya watoto wenye umri wa miaka chini ya mitano wapatao 18,313 sawa na Shilingi 3100.
Dkt.Linda amesema Watendaji wa Kata kwa kushirikiana na Viongozi wote ngazi ya Kata na wazazi wahakikishe wanafunzi wote mashuleni wanapata chakula cha mchana na asiwepo mwanafunzi ambaye hapati chakula.
Sima Mark Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Wajumbe mbalimbali wakifatilia kikao cha lishe katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Mafinga.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.