“ Niwapongeze sana Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Mji Mafinga kwa kuelekeza fedha nyingi kutekeleza Miradi ya Maendeleo Hasa kwa kupitia Mapato ya Ndani., Hamkuwa wabinafsi Miradi Mikubwa kwa kupitia mapato ya ndani imetekelezwa katika kipindi chenu, hili ni jambo kubwa la kujivunia kwenu na kutoa ushirikiano Mkubwa kwa Serikali “
Kupitia Mapato ya Ndani Halmashauri imeweza kujenga kituo cha Afya Bumilayinga, Shule ya Sekondari Upendo, Jengo la Wazazi zahanati ya Rungemba, wodi daraja la kwanza katika Hospitali ya Mji Mafinga na Miradi Mingine Mingi. Hakika Waheshimiwa Madiwani mna Haki ya kupongezwa.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa alipokuwa akitoa salamu za Serikali katika kikao cha BARAZA la Waheshimiwa Madiwani la robo ya tatu Januari- Machi lililofanyika Leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Mafinga.
Aidha amewataka kulinda Amani kubwa ya Nchi na Umoja walioujenga baina yao .Pia wasikubali kugawanywa hasa katika kipindi cha kuelekea katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025.
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.