Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe.Dkt.Linda Selekwa amefanya Kikao na Waandishi wa Habari katika Ofisi yake ya Wilaya ya Mufindi na Kuwahakikishia Usalama Wananchi kuelekea Uchaguzi mkuu Mwaka 2025.
Akiongea katika kikao hicho Mhe.Dkt.Linda Selekwa amesema Wananchi wajitokeze kupiga kura kwa sababu ni Haki yao Kikatiba na hakuna Mgombea wa kupita bila kupingwa kwa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
“Wananchi baada ya kupiga Kura hatutegemei Watu kukaa Vituoni na kulinda Kura na pia msikubali kusikiliza Maneno au Kuyumbishwa pia epukeni vitendo vitakavyohusisha Uvunjivu wa Amani pia Viongozi wa Dini Muwasihi Waumini wenu kulinda Amani na Utulivu”. amesema Mhe.Dkt .Selekwa.

Uchaguzi Mkuu Tanzania unafanyika kila baada ya Miaka Mitano na ni Tukio muhimu linalohusisha Wananchi kuchagua Raisi wa Jamhuri,Wabunge wa Bunge la Taifa na Madiwani.
Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa upande wa Tanzania bara mchakato mzima unasimamiwa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ambayo inahakikisha kila hatua inafanyika kwa Uwazi,Haki na Usawa.
Vedasto Faustine Malima
Afisa Habari
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.