BAJETI YA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024
Baraza la Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Mji Mafinga limepitisha Mpango wa Bajeti ya Halmashauri ya Mji Mafinga kwa mwaka wa fedha 2023/2024 yenye thamani ya TSH 29,312,377,819.00.
Akiwasillisha Taarifa mbele ya Waheshimiwa Madiwani Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu Ndugu, Apolinary Seiya kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi, Happiness Laizer amesema kuwa katika fedha hizo,
- Bilioni 6.790 ni kwaajili ya Miradi ya Maendeleo
-Bilioni 16.539 Mishahara
-Bilioni 5.982 Matumizi mengineyo .
Ameongeza kuwa katika mapato hayo Halmashauri inatarajia kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 6.283 mapato yake ya ndani ambapo Bilioni 1.388 ni mapato fungiwa na Bilioni 5.339 mapato Halisi.
Amevitaja vipaumbele vya Halmashauri vilivyojumuishwa kwenye Mpango na Bajeti wa mwaka wa fedha 2023/2024 kuwa ni:-
-Kuimarisha Utawala Bora kwa kuzingatia,demokrasia, Utawala wa sheria,
-Ukusanyaji wa Mapato
-Kutekeleza miradi mipya na kukamilisha miradi viporo katika sekta ya Elimu , Afya, Utawala na huduma za Jamii. Pia kuimarisha hali ya Usafi na Uhifadhi wa Mazingira.
Akizungumza Mwenyekiti Wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge amesema kuwa Bajeti hii ni rafiki kwa kuwa inagusa maisha ya watu moja kwa moja, kuboresha Miradi ya Maendeleo na kuongeza ukusanyaji wa mapato.
Sima Bingileki
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Halmashauri Ya Mji Mafinga.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.