Na: OR-TAMISEMI
Timu za mikoa ya Mwanza na Dodoma, zimeingia fainali ya soka Wavulana katika mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania Kitaifa Iringa.
Tumu hizo zimeingia fainali baada ya kupata ushindi kwenye michezo ya nusu fainali iliyochezwa asubuhi ya leo juni 17, 2025 hivyo kukata tiketi ya kucheza fainali inayotarajiwa kuchezwa juni 18,2025.
Katika uwanja wa shule ya Sekondari Lugalo, timu ya soka ya mkoa wa Mwanza umeifunga Dar es Salaam kwa goli 1-0, katika mchezo mkali na wa kusisimua matokeo ambayo yamefuta ndoto za Dar kushinda ubingwa wa soka wavulana kwenye UMITASHUMTA 2025
Nayo timu ya mkoa wa Lindi ulipoteza matumaini ya kucheza fainali kwa mara ya kwanza, baada ya kukubali kipigo cha magoli 4-1 kutoka kwa Dodoma.
Mashindano ya UMITASHUMTA yapo kwenye hatua za fainali na nusu fanali, kwa michezo mbalimbali, huku baadhi ya michezo kama riadha na Cricket ikiwa imeshakamilika na mabingwa kujulikana.
UMITASHUMTA na UMISSETA 2025 inafanyika kitaifa mkoani iringa, kwa usimamizi wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI ikishirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.