Mwenge wa Uhuru 2025 katika Halmashauri ya Mji Mafinga yazindua, kukagua na kuweka jiwe la Msingi katika Miradi 11 ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 3.1.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Miradi hiyo Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Ismail Ally Ussi amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora na haraka ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu katika sekta zote hasa Elimu, Afya na Maji, Barabara na Umeme.
“ Wananchi mliokusanyika hapa hakikisheni mnatunza Amani hii ya nchi na mkishiriki kutunza Miradi hii ya Maendeleo kwani imeletwa kwaajili yetu ikiwa ni matamanio ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuona huduma bora inatolewa kwa wananchi, kuanzia ngazi ya mtaa”
Miradi iliyozinduliwa kuwekewa jiwe la Msingi na kukaguliwa ni ujenzi wa nyumba ya mtumishi(2 in 1) katika Kituo cha Afya Ifingo, Ofisi ya Kata Kinyanambo, kukagua matumizi ya nishati Safi Pandamiti Kibiashara,Uzinduzi wa Kituo cha Mafuta cha Castoil, kuzindua bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalumu, Madarasa mawili na Mradi wa Maji katika Shule ya Msingi Amani, kukagua shughuli za vijana waliopata Mikopo Asilimia 10, barabara, uzinduzi wa wodi daraja la kwanza katika Hospitali ya Mji Mafinga, utunzaji wa vyanzo vya maji na kukagua eneo kwaajili ya ujenzi wa viwanja vya michezo.
Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Mufindi umepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa akiwa na Kamati ya Ulinzi Wilaya ya Mufindi, Mkurugenzi Mji Mafinga Bi. Fidelica Myovela. viongozi wa Chama Wilaya ya Mufindi, Viongozi wa Dini. Taasisi Mbalimbali na Wananchi wa Wilaya ya Mufindi.
Sima Mark Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.