MWENGE WA UHURU -2022 WAZINDUA, KUWEKA MAWE YA MSINGI NA KUKAGUA JUMLA YA MIRADI SABA YA MAENDELEO UKIWEMO MRADI WA UJENZI WA MADARASA MATATU SHULE YA SEKONDARI CHANGARAWE KWA( FEDHA ZA TOZO) ZA MIALA YA SIMU,YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 880,596,736.00 KATIKA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA.
Akipokea Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Mufidi Mheshimiwa Saad Mtambule amesema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa Kilometa 20.53 katika Mji wa Mafinga na kupitia Miradi saba ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi Milioni 880,596,736.00.
Ameitaja Miradi hiyo kuwa ni Kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa bweni katika Shule ya Msingi Amani, Kuzindua Mradi wa Maji katika Shule ya Sekondari Kinyanambo.
Kukagua mradi wa Uoteshaji miche bora ya Parachichi, Kukagua Mradi wa kikundi cha Vijana NESA, Kuzindua Mradi wa Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami Mtaa wa Mkombe, Kuzindua Mradi wa Ujenzi wa madarasa matatu na ofisi moja kwa fedha za tozo Shule ya Sekondari Changarawe na Kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Jengo la kutolea huduma za Dharura(EMD) katika Hospitali ya Mji Mafinga.
Akizungumza baada ya kukagua na kuzindua Miradi yote ya Maendeleo katika Mji Mafinga, Mkimbiza Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndugu Sahili Nyanzabara Geraruma amesema hakika Miradi iliyopitiwa, kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya Msingi inaendana na fedha iliyotumika kwani Miradi imetekelezwa kwa wakati na inagusa maisha ya wananchi moja kwa moja.
“ Hiki ndo kitu ambacho Serikali inataka kuona, ukiambiwa Jenga madarasa jiongeze ongeza na Ofisi ya walimu jambo hili mlilolifanya kwenye Shule ya Sekondari ya Changarawe limetugusa sana. Mlipokea kiasi cha shilingi million 37,500,000 kutoka Serikali kuu ikiwa ni Ukamilishaji wa Madarasa matatu fedha za Tozo, Halmashauri mmechangia kiasi cha shilingi Milioni 19,445,500 wananchi mlioni 3.7 mmejenga madarasa mazuri kwaajili ya wanafunzi kusomea. Hakika hamjamuangusha Mheshimiwa Rais wetu, tuwapongeze wasimamizi wa Mradi huu na miradi yote, Mkurugenzi wa Mji Mafinga hakika utekelezaji wa Miradi unaonekana” Sahili Nyanzabara Geraruma Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa.
Akitoa salamu kwa wananchi Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mji Mheshimiwa Cosato Chumi amesema Utekelezaji Mzuri wa Miradi ya Maendeleo unaonekana katika Mji wa Mafinga kwaajili ya Ushirikiano kubwa uliopo kati ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi, Waheshimiwa Madiwani, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na wataalamu ngazi ya Wilaya wakiongozwa na Mkurugenzi wake Bi, Happiness Laizer.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO-MAFINGATC
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.