Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Mh. Charles j. Makoga amewataka wananchi kupanda miti kwa wingi ili kujikinga na hali ya jangwa na mabadiliko ya tabia nchi ameyasema hayo katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika moja ya chanzo cha maji kilichopo changarawe mjini mafinga.
Lengo la Halmshauri kwa mwaka 2019 ni kuotesha miche 1,500,000 hadi sasa jumla ya miche 1,090,769 imepandwa katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri zikiwemo shule, vituo vya afya na kwenye mipaka yote ya taasisi hizo, miti iliyopandwa ni miti rafiki na maji(mivengi) miti ya matunda (parachichi),mapambo na kivuli ili kuhifadhi mazingira,kupendezesha maeneo ya wazi na kuhifadhi nyanzo vya maji lakini pia kuimarisha mipaka ya taasisi,kujipatia kipato na kuondokana na tatizo la utapiamlo katika jamii hususani kwa watoto wa shule.
“leo ni siku muhimu kwetu kwani umelenga kukumbushana na kuelimishana juu ya umuhimu wa kuhifadhi na kutunza mazingira kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo hivyo wito wangu kwa wananchi wote,vyombo vya habari,taasisi zote za serikali na asasi za kiraia na watendaji wote katika ngazi za Halmashauri ya Mji wa Mafinga kutekeleza kikamilifu sheria na kanuniza hifadhi za misitu na vyanzo vya maji,kuwepo na mikakati bora ya kuhifadhi vyanzo vya maji,mipango bora ya ardhi,mikakati ya kudhibiti uvunaji holela wa misitu pamoja na kilimo kisicho endelevu”alisema Mh. Makoga.
Serikali iliamua kutenga tarehe mosi aprili ya kila mwaka kuwa ni siku maalumu ya upandaji miti kitaifa lakini kwa kuzingatia tofauti za majira ya mvua kuanza na kuisha katika maeneo mbalimbali ya nchi Mkoa wa Iringa ulipanga uzinduzi wa upandaji wa miti katika maeneo ya mkoa kufanyika mwezi Januari kila mwaka na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Panda miti hifadhi mazingira na vyanzo vya maji kwa vizazi vya sasa na vya baadae”
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.