• Malalamiko |
    • Wasiliana na sisi |
    • Maswali |
    • Baruapepe |
Mafinga Town Council
Mafinga Town Council

Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mafinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Organization Structure
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Kilimo na umwagiliaji
      • Fedha
      • Mipango na Takwimu
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Afya
      • Ardhi na Maliasili
      • Community Development,Social welfare Gender and Youth
      • Water
      • Work
    • Vitengo
      • Community
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Huduma za Kisheria
      • Biashara
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa madiwani
    • Kamati Za Kudumu Za Halmashauri
      • Fedha Na uongozi
      • Mipangomiji Namazingira
      • Uchumi, Fedha Na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana Na Mwenyekiti
  • Miradi Mbalimbali
    • Progressive projects
    • Itakayo Tekelezwa
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Machapisho ya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Makitaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Malalamiko

Naibu Waziri Tamisemi aagiza bohari ya dawa na vifaa tiba kupeleka vifaa tiba kituo cha afya Ihongole

Posted on: August 1st, 2018

 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe Joseph George Kakunda ameitaka bohari ya dawa na vifaa tiba (MSD) kupeleka vifaa tiba mara moja katika kituo cha afya Ihongole kilichopo katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga mkoani Iringa.

Ameyasema hayo leo alipotembelea kituo hicho wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga na kukagua jengo la maabara na chumba cha upasuaji (Theatre)

Mh. Kakunda ameiagiza bohari ya dawa na vifaa tiba (MSD) kuhakikisha wanapeleka vifaa tiba haraka iwezekanavyo na kutoa muda wa mwezi mmoja kuhakikisha vifaa na madawa yanayotakiwa katika kituo hicho yanafika kwa wakati ili huduma muhimu zilizokusudiwa zianze kutolewa kwa wananchi.

“kituo chetu kimejengwa vizuri sana kwa viwango vyetu vya kitaifa, nimekagua chumba cha upasuaji nimeona kiko tayari kabisa kuanza kazi bado vifaa tiba tu” alisema Mh. Kakunda. 

 

Aidha aliwapongeza mkuu wa wilaya, mkurugenzi na wakuu wa idara kwa usimamizi mzuri, “kazi hii imefanyika vizuri sana mimi kwa kweli napeleka ujumbe kwa Mhe Makamu wa rais aliyeweka jiwe la msingi kwamba kituo kimekamilika vizuri hongereni sana” alisema Naibu Waziri Mh. Kakunda.

Upanuzi na ukarabati wa kituo cha afya Ihongole ulipangwa kutumia kiasi cha shilingi milioni mia tano  ambazo zote zimetolewa na Serikali kuu.

Utekelezaji wa mradi huu ulianza mwezi novemba 2017 mpaka sasa umegharimu kiasi cha shilingi milioni mia nne themanini na tano ambazo ujenzi na ukarabati upo kwenye hatua za umaliziaji, fedha iliyobaki kiasi cha shilingi milioni kumi na tano itatumika kuweka mfumo wa GOTHOMIS pamoja na umaliziaji wa malipo ya kazi ndogo ndogo zilizobakia.

Hali ya utoaji huduma katika kituo cha afya Ihongole ni nzuri na imeendelea kuimarika hususani baada ya kuongezeka kwa fedha zinazotumika kununua dawa.

Akisoma taarifa ya upanuzi wa kituo mganga mfawidhi wa kituo cha afya Ihongole bi. Proserpina Kalanje alisema lengo la mradi huo ni kupunguza vifo vya watoto wachanga na kinamama wajawazito kwa kuimarisha miundombinu na kuboresha huduma za Afya katika kituo ili kiweze kutoa huduma za upasuaji wa dharula na huduma ya kuongeza damu.

“Ili kufanikisha hilo mradi umelenga kuongeza majengo ya upasuaji, maabara na wodi ya wazazi lakini pia tuna changamoto ya uhaba wa watumishi kwani mpaka sasa kituo kina watumishi kumi na sita tu wakati mahitaji ni arobaini na tisa hivyo tunaiomba serikali kutuongezea watumishi ili wananchi waendelee kupata huduma bora zaidi” alisema bi. Kalanje.

Kituo hiki kilianza kutoa huduma mwaka 2008 ambapo kilikuwa kinahudumia wastani wa watu 5,000 kwa mwaka na kwa sasa kinahudumia wastani wa watu 26,032 kwa mwaka ikiwa ni ongezeko la wastani wa watu 21,032 kutoka katika kata jirani za kinyanambo, changarawe na isalavanu.

Matangazo

  • NAFASI ZA MASOMO KWA SHULE YA CHIEF MKWAWA ENGLISH MEDIUM- HALMASHAURI YA MJI MAFINGA. NAFASI BADO ZIPO TUPIGIE January 29, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA YANAPATIKANA www.mafingatc.go.tz July 13, 2024
  • MJI MAFINGA YAVUKA LENGO UKUSANYAJI MAPATO YAKUSANYA ASILIMIA 113 KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024 August 14, 2024
  • MATOKEO YA DARASAM LA SABA 2024 YANAPATIKANA KWENYE TOVUTI YETU .www.mafingatc.go.tz October 30, 2024
  • View All

Habari mpya

  • VITUO VYOTE VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA VIFUNGWE MFUMO WA GoT-HOMIS

    June 20, 2025
  • HALMASHAURI YA MJI MAFINGA YAPATA HATI SAFI YA UKAGUZI KUTOKANA NA TAARIFA YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (CAG) KWA HESABU ZINAZOISHIA TAREHE 30 JUNI 2024

    June 19, 2025
  • HALMASHAURI YA NKASI YAITEMBELEA MAFINGA MJI KUBADILISHANA UZOEFU

    June 18, 2025
  • MWANZA NA DODOMA ZATINGA FAINALI SOKA WAVULANA UMITASHUMTA 2025

    June 17, 2025
  • View All

Video

SENSA NI MAENDELEO
Video zaidi

Viungo Vya Haraka

  • Maelezo na Form Ya kiapo cha uadilifu
  • https://matokeo.necta.go.tz
  • Muongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya wananchi

Watembeleaji kidunia

world map hits counter

Idadi ya watu wanao tembelea Tovuti

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana na sisi

    Mafinga Town.

    Postal Address: Po.Box 76 Mafinga

    Simu: +255 262 772 393

    Mobile: 026-2772393

    Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.