“ Lengo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha wananchi wanaoishi Mjini wanapata Maji safi na salama kwa Asilimia 95 na vijijini Maji yanapatikana kwa asilimia 85. hivyo Mradi huu wa kuboresha mifumo ya Maji katika Mji Mafinga ni moja kati ya Miradi 28 inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita.
Akizungumza Naibu Waziri wa Maji (Mb) Mhandisi Kundo Andrea Mathew amesema
Mradi huu wa Maji wenye thamani ya shilingi Bilioni 48.06 Utasaidia kuongeza watumiaji wa Maji kufikia lengo la Mheshimiwa Rais la kuhakikisha kila mwananchi mjini na vijijini anapata Maji safi na Salama.
“ Mradi ni mzuri ila utekelezaji wake Umefikia asilimia 16 na ulitakiwa ukamilike Machi 2024 nimeona utekelezaji wa mradi na nitaenda kusukuma ili fedha zije haraka kukamilisha mradi huu ili malengo ya Mheshimiwa Rais yatimie ya kuhakikisha wananchi wanapata Maji safi na Salama Mjini na vijijini.
Mradi huu wa Maji utahudumia wananchi zaidi ya 95000 wa kata za Boma, Wambi, Changarawe, Upendo na unasimamiwa na MAUWASA Mkoa wa Iringa.
Mheshimiwa Naibu Waziri Mathew ametembelea Mradi eneo la jeshini yanapojengwa matenki ya Maji na baadae ametembelea Chanjo cha Maji na Amepokelewa na Kaimu Mkuu wa Wilaya Ndugu Frank Sichalwe na Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi, Fidelica Myovella na Wakuu wa Idara
Sima Bingileki
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Mafinga Tc
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.