OFISI ZA WASIMAMIZI WASAIDIZI ZIPO WAZI KUANZIA SAA 2:00 ASUBUHI NA ZITAFUNGWA SAA 12:00 JIONI KWAAJILI YA KUPOKEA MAPINGAMIZI-HALMASHAURI YA MJI MAFINGA
Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya Wilaya wakiongozwa na Msimamizi wa Uchaguzi Wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi Fidelica Myovella wamekagua na kuhakikisha Ofisi za Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi zipo wazi kupokea mapingamizi kutoka kwa wananchi wasioridhishwa na uteuzi wa wagombea nafasi mbalimbali uliofanyika tarehe 8 Novemba 2024 Siku ya Ijumaa.
Vituo vilivyotembelewa na Kata ya Boma, Isalavanu, Wambi, Rungemba
Vituo vyote vilikuwa wazi kuanzia saa 2:00 asb na vinatarajiwa kufungwa saa 12:00 Jioni.
Msimamizi wa Uchaguzi Wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi Fidelica Myovella akikagua na kuhakikisha Ofisi za Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi zipo wazi kupokea mapingamizi kutoka kwa wananchi.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.