“ Lengo la Serikali ni kuona Wawekezaji wanafanya shughuli zao Katika Mazingira mazuri hawabugudhiwi kwani uwepo wao unaongeza ajira kwa vijana wa kitanzania, kuongeza mapato na kuboresha mahusiano kati ya nchi na nchi.”
Pia tuhamasishe wananchi kutunza misitu yetu ya Asili, wasikate miti waweke Mazingira mazuri ya kuvutia kwa nyuki “
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego alipokuwa akifanya ziara ya kutembelea Wadau mbalimbali wa Maendeleo walio katika Mji wa Mafinga na kusikiliza changamoto wanazokabiliana nazo na kujua shughuli zinazofanywa na wadau hao.
Amesema Wadau wa Maendeleo ni nguzo kubwa ya maendeleo na Uchumi wa wananchi na Serikali hivyo Wadau wa maendeleo Hasa wa viwanda na ni muhimu kuwasikiliza kila wakati na kutatua changamoto wanazokabiliana nazo.
Mkuu wa Mkoa atakuwa na siku tano za kikazi Wilaya ya Mufindi na kesho anatarajiwa kufanya kikao na WAWEKEZAJI wa Viwanda katika Wilaya ya Mufindi.
Katika ziara yake leo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego ametembelea Shamba la Miti Sao Hill, Kiwanda cha Dazhong kinachozalisha Marineboards, Panda Miti Kibiashara na Kiwanda cha MDF.
Aidha Mkuu wa Mkoa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Saad Mtambule, Kamati ya Ulinzi ma Usalama Wilaya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga pamoja na Mkurugenzi wa Mji Mafinga na baadhi ya Wakuu wa Idara.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGA TC
Sima Bingileki
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.