Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe.Kheri James amefanya ziara katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga na kukagua ujenzi wa Barabara ya kiwango Cha Lami inayoanzia Mtaa wa Makondeko na kuishia Mtaa wa Ihongole.
Akizungumza na Wananchi pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga katika Mtaa wa Ihongole up Mhe.Kheri James amesema “Wananchi ni wajibu wenu kutunza Barabara kwa kuacha kutupa taka kwa manufaa yenu na vizazi vyenu kwa sababu inawasaidia katika usafiri,kurahisisha Shughuli za Maendeleo ya kiuchumi na inachochea ukuaji wa biashara”.
Akiambatana na Mkuu wa Mkoa katika Ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe.Linda Selekwa amesema kuwa Serikali inapambana katika Ujenzi wa Barabara kwa kiwango Cha Lami katika Mkoa wa Iringa hivyo Wananchi wanapaswa kuunga mkono jitihada za Serikali na Viongozi katika kuleta Maendeleo,pia ameipongeza TARURA kwa kusimamia Mradi wa Ujenzi .
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Ihongole ndugu Fasto Madenge amesema kuwa wanashukuru jitihada za Serikali katika kufanikisha Ujenzi wa Barabara na Taa ambazo zinawasaidia katika Shughuli za kiuchumi hivyo wanaahidi kulinda hiyo miundo mbinu. Mhe.Mkuu wa Mkoa ameendelea kumshukuru Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwasaidia kutekeleza Mipango mbalimbali ya Maendeleo katika Mkoa wa Iringa na ameipongeza Halmashauri ya Mji wa Mafinga chini ya Mkurugenzi Bi; Fidelica Myovella kwa ukusanyaji na matumizi Bora ya Fedha kwa kuzingatia vipaumbele kama Barabara,Elimu na Afya.
Vedasto Faustine Malima.
Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.