Mafundi wa kila jengo wapo na tunahakikisha vifaa vyote vinapatikana kwa wakati , yapo majengo yaliyokamilika na yale ambayo bado tunahakikisha mpaka kufika tarehe 30 Disemba , 2024 majengo yatakuwa yamekamilika kwaajili ya kupokea wanafunzi wa kidato cha Kwanza 2025.”
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mji Mafinga Bi. Fidelica Myovella alipokuwa akifanya Ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Upendo, Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Amali( Ufundi)Changarawe na Ukamilishaji wa Majengo ya ICU, Maternity Complex na Jengo la kufulia katika Hospitali ya Mji Mafinga.
Amesema kikubwa kinachozingatiwa ni matumizi Sahihi ya Fedha, Ubora wa Mradi na Ukamilishaji wa Mradi kwa Wakati ili kuleta Tija kWa watumiaji na kufikia malengo ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha huduma bora Zinatolewa kwa kila sekta.
Imeandaliwa na Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu Halmashauri ya Mji Mafinga.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mafinga Mji Bi Fedelica Myovella akikagua madarasa ya shule ya sekondari Upendo ambayo yanatarajia kuanza kupokea wanafunzi mwezi wa kwanza.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.