“ Mmeona jinsi ambavyo TAKUKURU Wilaya ya Mufindi wanafanya kazi kwa Uaminifu , Kuokoa kiwango cha shilingi Milioni 21 na Ellf Arobaini kwa wananchi sio jambo dogo, Hili liwe fundisho kwetu wananchi.Rudisheni imani kwa TAKUKURU na Serikali”
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu anatutaka tutatue kero za wananchi na kuwasikiliza tunafanya hivyo kama Serikali na nyie wananchi jukumu lenu lipo pale pale toeni taarifa kuhusu uhalifu, Tufichue uhalifu ni jukumu lako na jukumu langu”
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa alipokuwa akikabidhi kibali cha kuendelea na matumizi ya fedha kiasi cha shilingi 21,000,40.00/- baada ya fedha hizo kuokolewa na TAKUKURU- MUFINDI na Mahakama kuamuru fedha hizo zirudi kwa wananchi kwaajili ya Matumizi ya Serikali ya kijiji cha Matanana katika Halmashauri ya Mji Mafinga fedha ambazo zilitokana na Mauzo ya Miti.
Amesema TAKUKURU Wilaya ya Mufindi imekuwa ikifanya kazi kwa uaminifu Mkubwa hili linawadhihirishia wananchi kuwa tunatakiwa kurudisha imani kwenye chombo hiki na Serikali kuwa kazi inafanyika.
Naye Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Mufindi Bw. Abdull Abdarahman amesema lengo na jukumu la TAKUKURU ni kuhakikisha Fedha na mali za Serikali zinatumika ipasavyo kwa madhumuni husika na fedha zinazotekeleza Miradi zinatumika kwa lengo kusudiwa nakwa uhalisia na Miradi inafanya kazi ipasavyo.
Amesema TAKUKURU imepambana, kusimamia na kurejesha fedha kwenye kijiji ili zitumike kwenye matumizi mengine na tukiona kuna dhana ya vitendo vya rushwa kwenye jamii tunafuatilia baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi.
Aidha kikao hicho kimehudhuriwa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa Ndugu Victor Swela na timu kutoka Mkoani, Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Mufindi na Kaimu Mkurugenzi Mji Mafinga Ndugu Charles Mwaitege.
“kuzuia rushwa ni jukumu langu na lako tutimize wajibu wetu”
Imeandaliwa na Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mji Mafinga
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.