Mh.Dr Marry mwanjelwa waziri wa kilimo amewataka wafanyabishara na mawakala kufuata bei elekezi ya serikali na kuachana na tamaa ya kutaka kupata faida kubwa, serikali ya awamu ya tano ina mipango thabiti ya kumkomboa mkulima kwa kufufua vyama vya ushirika.Serikali inawapokea na kuwajali wawekezaji lakini pia na wawekezaji wana wajibu wa kuhakikisha wanaingia mkataba na wakulima ili kuepuka malalamiko mbalimbali toka kwa wakulima na pia wakulima wenyewe kujinga kwa pamoja na na kuanzisha vikundi vya wakulima kwani kwa kufanya hivyo itawasaidia wakulima kudai haki zao mbalimbali kama vile bei ya mazao na mengine, pia itakuwa rahisi kwa Serikali kuweza kuwafikia kwa urahisi zaidi pindi jambo lolote, aidha Serikali kwa sasa iko kwenye mpango wa kuleta bei elekezi ya zao la chai na pareto.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.