Mh. Merdad Kalemani alitoa agizohilo alipofanya ziara ya kutembelea viwanda vinavyochakata nguzo za umeme katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga,katika ziara yake hiyo Mh.Kalemani alitembelea viwanda viwili vya kuzalisha nguzo za umeme na kushuhudia uzalishaji mkubwa wa nguzo hizo ‘’naangiza ni marufuku kuanzia sasa kwa makampuni kuagiza au kununua nguzo za umeme kutoka afrika kusini kwa kampuni yoyote itakayo agiza nguzo kutoka nje ya Nchi hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake,Serikali ya awamu ya tano inaanzakutekeleza mpango wa usambazaji wa umeme vijijini REA awamu ya tatu na itachukua siku saba tu kwa mwananchi kupata umeme toka siku ya maombi yake ya kuingiziwa umeme kwa hiyo Serikali haitapenda kuona juhudi hizi zinakwama kwa kisingizio cha kukosa nguzo za umeme’’
Katika ziara hiyo Mh. Waziri wa nishati alilidhishwa na kasi nzuri ya uzalishwaji wa nguzo za umeme kwa kutembelea kiwanda cha Qwihaya chenye uwezo wa kuzalisha nguzo laki tatu (300,000) kwa mwaka na baadae kutembelea kiwanda cha Sao-hill chenye uwezo wa kuzalisha nguzo laki mbili na hamsini (250,000).Aidha Waziri pia alitoa rai kwa wananchi kutunza miundombinu kwa kutochoma moto msitu.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.