Lengo la TAKUKURU Wilaya ya Mufindi ni kuhakikisha nyaraka zote muhimu za Miradi zipo na hakuna Mradi hata mmoja utakaokataliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 tunahakikisha kasoro zote tunazibaini na kuwafikishia wahusika ili wazifanyie kazi “
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Mufindi Bw. Abdull Abdarahman na Timu yake walipotembelea na kukagua nyaraka kwenye Miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru tarehe 1 Mei, 2025 katika Halmashauri ya
Mji Mafinga.
Katika Ziara hiyo TAKUKURU Wilaya ya Mufindi imepitia Mradi wa Ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi katika Kituo cha Afya Ifingo, Ofisi ya Kata Kinyanambo, Bweni katika Shule ya Msingi Amani, ( Mahitqji Maalumu)Mradi wa Maji na Mradi wa Ujenzi wa Madarasa 2 Shule ya Msingi Amani, Mradi wa Barabara, Mazingira Soko Kuu Mafinga na Mradi wa Wodi Daraja la Kwanza katika Hospitali ya Mji Mafinga.
Kwa Upande wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mratibu wa Mwenge Ndugu Henry Kapella akimuwakilisha Mkurugenzi wa Mji amepokea maekekezo na kuahidi kuwasiliana na wahusika ili kuyafanyia kazi kabla ya Mwenge Kupita.
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.