Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Wilaya ya Mufindi kimetoa vifaa vya michezo ikiwemo Mipira na Jezi zilizokabidhiwa na Rugatekanisa Atenodurus Isidory Mwenyekiti wa Kamati ya Uratibu Talgwu Mafinga Mji akiwa ameambatana na Veneranda Ngalali
Katibu kamati ya Uratibu Talgwu kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga.
Akipokea vifaa hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi, Fidelica Myovella amewashukuru kwa mchango wa Vifaa hivyo na amesema vitaenda kutumika kwenye Mashindano ya michezo SHIMISEMITA Tanga na kusaidia katika Michezo siku zijazo.
SHIMISEMITA ni Shirikisho La Michezo Serikali za Mitaa Tanzania ambapo kwa Mwaka 2025 Mashindano ya Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa yanatarajiwa kuanza 15/08/2025 mpaka 29/08/2025 mkoani Tanga.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.