Timu ya Hamasa toka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imefika leo Tarehe 17/12/2024 katika Halmashauri ya Mji Mafinga kuhamasisha Wananchi kujitokeza katika kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2025. Zoezi hili litafanyika kuanzia Tarehe 27 Disemba 2024 mpaka 2/1/2025
Akizungumza George Kashura Afisa wa tume amewataka Wananchi kuzingatia sifa za kujiandikisha kwa Mpiga Kura ambazo ni:-
1. Awe raia wa Tanzania.
2. Awe ametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea.
3. Awe hajapoteza sifa kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi au Sheria nyingine zilizotungwa na Bunge.
Pia amechukua nafasi iyo kuwakumbusha zoezi linawausisha wanaojiandiksha mara ya Kwanza lakini pia linawahusu wale ambao walijiandikisha awali na amehama eneo moja la Uchaguzi kwenda lingine anatakiwa aje aweke taarifa zake za sehemu alipo kwa sasa na
Aliyepoteza au Kadi yake kuharibika wafike katika Kituo cha kujiandikisha.
Muda kitafunguliwa saa 2:00 asubui na kufungwa saa 12:00 jioni.
“KUJIANDIKISHA KUWA MPIGA KURA NI MSINGI WA UCHAGUZI BORA”
Na
Ana Mdehwa
Picha mbalimbali za kuhamasisha wananchi kujitokeza na kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.