Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya MJI ikiongozwa na Mkurugenzi wa MJI Mafinga Bi. FIDELICA MYOVELLA imefanya ziara ya Ufuatiliaji kwenye Mradi wa Umwagiliaji wa Mtula kuona shamba darasa linalosimamiwa na Idara ya kilimo Mji Mafinga linavyoleta tija kwa wakulima wa eneo hilo .

Akizungumza Mkurugenzi Mji Mafinga Bi Fidelica Myovella amesema mkakati wa Halmashauri ni kuhakikisha wakulima wanapata faida kwenye kilimo katika Mfereji huo ambapo mazao yanayolimwa ya muda mfupi ni Vitunguu, hoho, viazi na nyanya .
Mkulima wa vitungu anayenufaika na mfereji huo wa Umwagiliaji ndugu Gilbert Longo amesema ni mala yake ya kwanza kulima na ushauri kuhusu kilimo cha vitunguu anapata kutoka kwa wataamu wa kilimo wa Halmashauri ya Mji Mafinga na mpaka sasa ameona mazao yanaendelea vizuri na ana uhakika wa kuvuna baada ya kupata ufahamu kupitia shamba darasa katika eneo hilo ambalo linasaidia wakulima wote wanaotumia mfereji huo wa umwagiliaji.

Miradi huu umejengwa na Fedha kiasi cha shilingi Milioni 500 kutoka Serikali Kuu na unahudumia zaidi ya wakulima 200 na Kilimo kinachofanyika katika eneo hilo ni Kilimo cha Mahindi, maharage, vitunguu viazi na nyanya.
“Tuwasaidie wakulima wapate tija kwa kuwa na mfereji huu wa mtula ili waweze kupata mazao mengi na bora” Amesema Bi. Fidelica Myovella
Aidha Mkurugenzi wa Mji Mafinga akiwa na baadhi ya wakuu wa Idara ametembelea Shamba la parachichi na kujionea maendeleo ya mradi huo,
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.