Timu ya Wataalamu kutoka “Mama Samia Legal Aid Campaign ( MSLAC) imewasili katika Halmashauri ya Mji Mafinga na kuahidi kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi bure kwa siku 10 kuanzia tarehe 11 Disemba- 19 Disemba 2024 katika Kata zote 9.
Akizungumza Kiongozi wa Timu hiyo Ndugu, Nicodemus Nditi amesema msaada huo wa huduma za Kisheria unatolewa bure kwa wananchi wote na unalenga kuwasaidia kutatua changamoto za kisheria wanazokutana nazo katika sekta za ardhi, ukatili, mirathi na Ndoa.
Naye Mratibu wa zoezi hili kwa Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu Elias Msuya amesema zoezi linaanza katika kata ya Bumilayinga na Isalavanu na tarehe 19 Disemba zoezi litahitimishwa kwa kuwa wananchi wengi watakuwa wamefikiwa kama ambavyo lengo la Mheshimiwa Rais linataka kuwa wananchi wapate huduma za kisheria bure mpaka ngazi ya kijiji.
Timu ya Mama Samia Legal Aid Campaign imepokelewa na Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi. Fidelica Myovella
Imeandaliwa na Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Mafinga TC
Picha ya pamoja na Wataalamu kutoka “Mama Samia Legal Aid Campaign ( MSLAC) ambao imewasili katika Halmashauri ya Mji Mafinga na kuahidi kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi bure kwa siku 10 kuanzia tarehe 11 Disemba- 19 Disemba 2024 katika Kata zote 9
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.