Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imeendesha mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura kwa awamu ya pili mafunzo kwa waandishi wasaidizi na waendesha kifaa cha bayometriki jimbo la mafinga mjini.
Afisa Mwandikishaji wa jimbo la Mafinga Mjini Ndugu Charles Mwaitege ametoa rai kwa waandishi wasaidizi na waendesha BVR kuwa waadilifu kwa serikali kwa kuhakikisha wanaelewa mafunzo haya kwa umakini mkubwa ili kuweza kufanikisha zoezi hili kubwa ambalo lipo mbele yetu.
Aidha Afisa Mwandikishaji Ndugu Mwaitege amesema kuwa Uboreshaji kwa Halmashauri ya Mji wa Mafinga zoezi hili litachukua siku saba katika vituo vyote ambavyo vilitumika awali kujiandikisha pia ametaka kuwa makini katika kutunza vifaa vya tehama kutunzwa kwa umakini na pia kuhakikisha fomu zote ambazo wapewa mafunzo wanazitumia vizuri kwa kujaza taarifa sahihi na kwa usafi bila kuharibu fomu hizo.
Pia amewataka kuhakikisha waandishi wasaidizi na waendesha BVR kukaa kwenye vituo vyao na kufungua mapema ili kuweza kuwahudumia wananchi ambao watajitokeza kuboresha au kuhamisha taarifa zao.
Michael Ngowi
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.