Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetoa mafunzo ya matumizi ya mashine ya kibayometriki kwa waandishi wasaidizi na BVR opareta ngazi ya Kata katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Halmashauri ya Mji Mafinga.
Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo washiriki wote ili kuhakikisha zoezi hilo la uwandikishaji na uboreshwaji wa taarifa katika daftari la kudumu la mpiga kura linafanikiwa kikamilifu kama lilivyo kusudiwa katika mafunzo hayo ambayo yamejikita katika matumizi sahii ya mashine ya BVR na ujazaji wa fomu na uhamishaji wa taarifa kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine.
Washiriki wa mafunzo hayo wametakiwa kuwa makini na kupokea mafunzo haya kwa umakini sabubu ndio msingi mkubwa kuelekea uchaguzi wa mwakani 2025 hivyo tunawajibu wakujua kutumia vizuri mashine hizi na ujazaji wa fomu hizi kwa umakini ili tuweze kuwahudumia wananchi vizuri kwenye maneo yao.
Hata hivyo waandishi wasaidizi na BVR opareta wamekumbukushwa kushirikiana kwa ukaribu pindi wanapokuwa katika vituo vyao ili kuhakikisha wanatoa huduma nzuri kwa wananchi ambao watakuwa wanajitokeza katika kuboresha na kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura na pia wameaswa kufuata miongozo na kanuni ambazo zimetolewa na tume huru ya taifa ya uchaguzi katika zoezi hilo ambapo zoezi hili linatarajia kuanza 27 Disemba 2024 kwa Halmashauri ya Mji Mafinga.
Michael Ngowi
Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.