Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mheshimiwa Asina Abdallah Omary amefungua mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa wasimamizi ngazi ya jimbo Halmashauri ya Mji Mafinga mafunzo hayo yamehudhuriwa na Watendaji wa Kata (ARO,s KATA ) na Waandikishaji wasaidizi ngazi ya Jimbo .
Mheshimiwa Jaji Asina Abdallah Omary amewapongeza Watendaji wote wakata kwa kuaminiwa na kuteuliwa na kuapa kwaajili ya kufanya kazi hii kwa uadilifu na uzalendo mkubwa amewaeleza umuhimu wa mafunzo haya na kuyaelewa ili yaweze kufanyika kwa ukamilifu mkubwa katika maeneo yetu hivyo ARO KATA mnawajibu wa kuyajua mafunzo haya ambayo ni matumizi ya mashine ya Bayometriki (BVR Kit) na ujazaji wa fomu mbalimbali kwa umakini mkubwa na kuwa makini kwa kusoma vitabu na makabrasha yaliyo tolewa na Tume .
Amewasisitiza ARO KATA na Waandikishaji wasaidizi ngazi ya Jimbo kuhakikisha wanafanya kazi kwa kufuata kanuni na sheria na kuacha kufanya vitu ambavyo havipo katika kanuni na sheria pia kujibu maswalli ambayo watakuwa wanaulizwa na wananchi ambao watakuwa wanajiandikisha katika maeneo yao na kutoa elimu juu ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ili kujenga uwelewa kwa wananchi , hata hivyo amewataka watendaji wote kuhakikisha wanalinda na kuvitunza vifaa hivi kwa umakini mkubwa kwani vifaa hivi ni vya gharama kubwa sana Serikali imetoa pesa nyingi hivyo tuna wajibu wa kuvitunza ili vikatumike kwa wengine.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi Fedelica Myovella ameshukuru kwa nasaha ambazo zimetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mheshimiwa Asina Abdallah Omary kwa ARO KATA na Waandikishaji ngazi ya Jimbo pia amesema Halmashauri itahakikisha inasimamia na kuendesha zoezi hili kwa umakini na ushirikiano mkubwa ili kuwafikia wananchi wote kwenye maeneo yao ambayo watakuwa wanaboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga kura .
Michael Ngowi
Afisa Habari Halmashauri ya Mji Mafinga.
Wajumbe wakifatilia mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa wasimamizi ngazi ya jimbo Halmashauri ya Mji Mafinga mafunzo hayo yamehudhuriwa na Watendaji wa Kata (ARO,s KATA ) na Waandikishaji wasaidizi ngazi ya Jimbo .
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.