Tume Huru yaTaifa ya Uchaguzi imeendesha mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata katika Jimbo la Mafinga Mjini ambayo yameanza leo na yanatarajiwa kumalizika tarehe 6 Agosti.
Akifungua mafunzo hayo Msimamizi Ngazi ya Jimbo Mwalimu Doroth Kobelo amewataka washiriki kuhakikisha wanafatilia na kuelewa mada zote ambazo zitafundishwa katika mafunzo haya ili kuweza kukuza uwelewa kuelekea uchaguzi Mkuu.
Aidha amewataka washiriki wa mafunzo haya kufahamu kuwa uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali za kikatiba na kisheria ambazo zinapaswa kufuatwa na kuzingatiwa ili kupunguza na kuondoa kabisa malalamiko au vurugu wakati wote wa mchakato wa uchaguzi.
Pia ametoa rai kwa washiriki wa mafunzo kuhakikisha wanafuta maelekezo ambayo yanatolewa na viongozi wa Tume ya Uchaguzi na wasimamizi wa Uchaguzi ili kuweza kukuza utendaji na uwajibikaji kwa kipindi chote cha Uchaguzi ikumbukwe mafunzo haya yanajumuisha washiriki 18 kutoka Kata 9 za Halmashauri ya Mji Mafinga ambao ni wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata.
Michael Ngowi Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.