“ Mashujaa wa Nchi yetu walipigani Umoja, Uhuru na Amani, hivyo ni wajibu wetu sisi kulinda Amani na kutunza maadili tuliyoachiwa ili kuwaenzi Mashujaa hao walio toa rehani Maisha yao kwa ajili Nchi yetu”
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa ambapo Kiwilaya Maadhimisho yamefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Mafinga kwa kuwaombea Dua Mashujaa waliopigania Uhuru na Amani ya Nchi yetu.
“Tusimame katika Misingi ya kutunza maadili na kutunza Amani ya nchi yetu, mashujaa wetu wamepigania nchi na Uhuru na wametoa rehani maisha yao, hebu tuwaenzi kwa kufanya kazi kwa bidii, kutunza maadili yetu na kukataa uvivu.”
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele katika kuenzi na kudumisha mila za nchi na utamaduni wetu ikiwa ni pamoja na kulinda Maadili yetu. Tuungane nae kila mmoja kwa nafasi yake atimize wajibu wake. Kwa kufanya hivi Taifa letu litakuwa salama.
Katika Maadhimisho hayo ya Siku ya Mashujaa Dua mbalimbali zimefanyika kuwaombea mashujaa wetu kutoka kwa viongozi wa dini.Dua hizo zimeongozwa na
Sheikh Adam Kavenuke Katibu wa Bakwata Wilaya ya Mufindi,Mchungaji Josephat Mtweve na Askofu William Ambakisye.
Aidha Nae, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge amesema kuwa dhamira zetu zitukumbushe tuone tunafanya nini kwaajili ya Taifa letu.
Aidha Maadhimisho hayo yameadhinishwa kwa kutolewa historia fupi ya Mashujaa, Dua kutoka viongozi wa Dini na hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt Linda Salekwa na Kuhudhuriwa na Katibu Tawala Wilaya ya Mufindi Ndugu, Frank Sichalwe, Mkurugenzi wa Mji Mafinga Ndugu, Ayoub Kambi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ndugu, Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, viongozi wa dini pamoja na watumishi Halmashauri za Wilaya ya Mufindi.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-MAFINGA TC
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini-Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.