“Tuwe na wajibu wa kuwafundisha na kuwaelekeza vijana kuhusu uvumilivu na kuchukuliana kwenye ndoa”
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Mufindi ndugu Reuben Chongolo akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa Halmashauri ya Mji Mafinga yaliyoadhimishwa kwa maandamano, maonyesho na jumuiko katika ukumbi wa CCM wilaya ya Mufindi.
Amesema wanawake wengi hawana uelewa katika fursa za kuwekeza , kumiliki na kutumia mali wanazozizalisha zaidi ya wao kuwa chombo cha kuzalisha mali tu.
Naye Katibu wa Kamati ya Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani Bi. Zeida David Sombe akisoma risala ya wanawake wa Mji Mafinga kwa Mgeni Rasmi amesema wanawake wa Mji Mafinga wanatamani kuwe na mgawanyo sawa wa uzalishaji mali na mgawanyo wa majukumu kwa wanawake na wanaume kwani mzigo mkubwa wa utunzaji wa familia umeachwa kwa mwanamke hivyo kupelekea mwanamke kushindwa kushiriki katika masuala ya kimaendeleo
Katika maadhimisho hayo Elimu ya Ukatili wa kijinsia imetolewa na Dawati la Jinsia kutoka Polisi Mufindi, Elimu kutoka Mucoba, SAOHILL, Panda miti kibiashara, RDO na kubudhuriwa na Wanawake kutoka makundi mbalimbali kutoka katika kata zote 9 za Halmashauri ya Mji Mafinga.
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Wanawake wa Halmashauri ya Mji Mafinga wakionsha shughuli za ujasiriamali katika siku ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.