UFUGAJI WA SUNGURA WABORESHA MAISHA YA MNUFAIKA WA TASAF-MAFINGA TC
Bi Angelamise Matandala (61) Mjane, mkazi wa Mjimwema katika Halmashauri ya Mji Mafinga Kata ya Boma anawatoto wawili walemavu wa akili mmoja wa Kike na mwingine wa kiume. Bi, Angelamise analea na kuhudumia watu 8 kwenye kaya yake na ni mnufaika wa Mpango wa TASAF-MAFINGA.
“Nimeweza kujenga nyumba hii ya bati japo haijaisha kutokana na Mpango wa kunusuru kaya maskini(TASAF) nikipata pesa nafuga,nalima vinyungu nauza mboga na nikipata pesa ndo nafanya mambo haya makubwa”
Baada ya kupokea fedha kutoka TASAF Bi, Angelamise ameweza kufuga sungura 12ambapo akipata fedha baada ya kuuza Sungura fedha hizo anajenga kuongeza mtaji wa sungura na fedha anazozipata kwenye kilimo zinaongeza kipato na kufanya maendeleo ya familia.
“ Mpango huu wa TASAF Umenisaidia mno nimejenga japo nyumba sijamaliza, ninalima ninafuga yaani tangu mpango huu umeanza 2020 nipo kwenye Mpango hakika mpango huu natamani uendelee. Namshukuru mama Samia Suluhu Hassan kwa kubali kutukoboa sisi wananchi wa hali ya chini.”
Aidha Bi, Angelamise anajishughulisha na kilimo cha bustani ya mboga mboga inayomsaidia kwa chakula na kuongeza uchumi wa familia yake. Ameongeza kuwa kwa sasa anashamba hekari moja ambapo analima mahindi, viazi na njegele akiuza mazao hayo anapata fedha zinazomsaidia kwa chakula na kufanya maendeleo.
Akizungumza na mwandishi wa Habari hizi Mtendaji wa Mtaa Mjimwema Bi Anna Masoud amesema kuwa katika mtaa wa Mjimwema kuna wanufaika 52 ambao wengi wao ni wale wanaojishughulisha na kilimo, mbogamboga, ufugaji na kuendeleza makazi.
Amesema kwa kuwa umri wake umesogea hawezi kujishughulisha na Mpango wa Ajira za muda kwa walengwa hivyo, binti yake anaenda kufanya shughuli hiyo na kupata malipo ya shilingi 30,000/- kwa mwezi.
Naye Mratibu wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini (TASAF III)Mafinga TC, Bwana stephen Mwendi amesema kuwa tangu mpango umeanza kwa Halmashauri ya Mji Mafinga, kuna jumla ya Kaya 1386
Na fedha zilizopokelewa kwa kipindi cha Septemba - Oktoba ni shilingi Milioni 41,918,200/- na Mpango unatelelezwa kwa kaya zote 9 za Halmashauri ya Mji.
Amesema Mpango umesaidia familia nyingi kupiga hatua za maendeleo kwani 80% ya kaya nufaika wanasomesha, wanajikimu na kipato cha familia zao kimeongezeka kwa upande wa uchumi.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-MAFINGATC
Sima Bingileki
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-MafingaTC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.