UJENZI WA JENGO LA WAGONJWA WA DHARULA (EMD) KUBORESHA UTOAJI HUDUMA-MAFINGA TC.
Ujenzi wa Jengo la dharula Hospitali ya Mji Mafinga unalengo la kuboresha Utoaji wa huduma za dharula pamoja na Kupunguza vifo vitokanavyo na majanga ya dharula ikiwemo ajali. Jengo hili la kutoa huduma za dharula katika Hosdpitali ya Mji Mafinga lilianza kujengwa tarehe 24/2/2022 baada ya Mji Mafinga kupokea fedha kutoka Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 kiasi cha shilingi Milioni 300.
Akizungumza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Utawala amesema Mkurugenzi wa Mji Bi, Happiness Laizer na wataalamu wake wanastahili pongezi kwani Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo unafanyika kwa umakini na kasi kubwa na thamani ya Miradi inaendana kabisa na fedha zilizotumika katika miradi husika.
Aidha, ameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha katika Halmashauri ya Mji Mafinga kwaajili ya Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Mji Mafinga imeahidi kutoa ushirikiano wakati wowote kwa Mkurugenzi na Timu yake pale watakapo hitaji ushauri ili kuhakikisha Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Mji wa Mafinga inatekelezwa kwa kuzingatia muda husika na kwa ubora.
Jengo la EMD katika Halmashauri ya Mji Mafinga linatarajiwa kutoa huduma zifuatazo:-
Huduma za Dharula.
Huduma za Upasuaji Mdogo.
Huduma za wagonjwa wa nje.
Huduma za Dawa na huduma za Mapumziko kwa wagonjwa.
IMEANDALIWA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO-MAFINGA TC
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.