Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya afya, hususan katika kuboresha miundombinu ya utoaji huduma kwa wananchi. Moja ya mafanikio makubwa katika Halmashauri ya Mji Mafinga ni ujenzi wa wodi ya daraja la kwanza (Grade One) katika Hospitali ya Mji Mafinga.
Mradi huu umejengwa kwa pesa za mkopo kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambao unalipwa na fedha za Mapato ya ndani ya halmashauri na hadi kukamilika kwake umetumia kiasi cha TSh 158,751,345.99.
Mradi huu ulianza rasmi tarehe 30 Novemba 2023, na ulijumuisha ujenzi wa wodi yenye vyumba nane (8) za daraja la kwanza na umezinduliwa rasmi kupitia mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa tarehe 01/05/ 2025, ikiwa ni ishara ya dhamira ya Serikali kuboresha afya ya wananchi wake kwa vitendo.
Ujenzi wa wodi ya daraja la kwanza umelenga, Kuboresha na kuongeza miundombinu ya kisasa ya kutolea huduma za afya. Katika Hospitali ya Mji Mafinga na kuendana na mahitaji ya wateja kwa sasa waliopo.
Kukamilika kwa Mradi huu umesaidia kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya kwa Wananchi wa Mji Mafinga na maeneo ya jirani.
Na,
Anna Mdehwa,
Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.