Timu kutoka Mikoa mbalimbali nchini imeanza kuwasili Mkoani Iringa kwaajili ya kushiriki Mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA ambayo yataanza tarehe 8/6/2025 Mpaka tarehe 30/6/2025.
Akizungumza Afisa Michezo na Utamaduni Mkoani Geita Ndugu. Bahati Rodgers amesema, kutoka Mkoa wa Geita wanafunzi waliowasili ni 120 na walimu 16 na daktari mmoja ambapo wanasichana ni 59 na Wavulana ni 61 ambao watashiriki michezo yote na hasa kutetea Ubingwa wao wa mwakq 2024
“ Tunashukuru tumepokelewa vizuri na maandalizi hakika yanaendelea vizuri, tuipongeze kamati ya maandalizi na Wizara ya OR- TAMISEMI wanafunzi wamepata malazi na walimu pia. Kikubwa hapa ni kutetea Ubingwa maana mwaka jana 2024 kwemye UMITASHUMTA tulikuwa na vikombe 4 na UMISSETA makombe 3 na zaidi mwaka huu tumeongeza kushiriki Soka Maalumu na riadha na kurudi na ushindi Geita”
Nae Afisa Utamaduni Mkoa wa Songwe Ndugu
Godfre Atumigwe Msoka amepongeza maandaliza na mapokezi ambayo wamepata tangu wamefika Mkoani Iringa kushiriki Mashindano hayo .
Ameongeza kuwa Timu kutoka Songwe wamewasili wanafunzi 120 wakiwamo walimu 14 na watashiriki Michezo yote kwani wanatetea ubingwa wa Netbali nafasi ya pili na Mpira wa mikono kwa wavulana nafasi ya kwanza kwenye UMITASHUMTA 2024
Mashindano haya yanatarajiwa Kuzinduliwa na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa na viwanja vitakavyo tumika kwenye michezo hiyo ni viwanja vya Shule ya Sekondari Lugalo, Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Iringa na Viwanja vya Chuo cha Walimu Kreluu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.