Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga, Bi. Fidelica Myovella, amezungumza na watumishi wapya wa Idara ya Afya waliopata ajira hivi karibuni, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kikazi, kufanya kazi kwa umoja na mshikamano, pamoja na kuwa daraja la huduma bora kwa wananchi.
“Twende tukafanye kazi, siyo kushindana. Tuwe wasikivu na si kutengeneza vizuizi, bali tuwe daraja la wale tunaowahudumia,” Amesema Bi. Fidelica, akihimiza maadili mema ya utumishi wa umma.
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Mafinga Dkt. Bonventula Chitopela, aliwakumbusha watumishi hao kuzingatia taratibu, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma, na kuwahimiza kutafuta ufafanuzi pale wanapokutana na changamoto na kutoa taarifa kwa mamlaka husika badala ya kufanya maamuzi bila uelewa wa kutosha .
Pia Katibu wa Afya Gusebius Ngatunga amewaeleza wasisite kutoa ushauri katika swala lolote pale wanapoona wanaweza kuboresha zaidi kwani inawezekana wakawa na uzoefu mzuri katika jambo fulani hivyo wawe huru kutoa mawazo yao.
Naye Muuguzi Mkuu wa Halmashauri ya Mji Mafinga Verichita Mchami amesisitiza kila mtu ahakikishe analeseni hai ya kutoa huduma ya Afya na pia wazingatie maadili ya wauguzi kwa kutoa huduma yenye staha.
Na,
Anna Mdehwa.
Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.